Deuteronomy 15:1-6

Mwaka Wa Kufuta Madeni

(Walawi 25:1-7)

1 aKila mwisho wa miaka saba ni lazima mfute madeni. 2Hivi ndivyo itakavyofanyika: Kila mkopeshaji atafuta mkopo aliomkopesha Mwisraeli mwenzake. Hatamtaka Mwisraeli mwenzake au ndugu yake amlipe hilo deni, kwa sababu wakati wa Bwana wa kufuta madeni umetangazwa. 3 bUnaweza kudai malipo kwa mgeni, lakini lazima ufute kila deni ambalo unamdai ndugu yako. 4 cHata hivyo, hapatakuwepo maskini miongoni mwenu, kwa kuwa katika nchi Bwana Mwenyezi Mungu wenu anayowapa kuimiliki kama urithi wenu, atawabariki sana, 5 dikiwa tutamtii Bwana Mwenyezi Mungu wenu kikamilifu na kuwa waangalifu kuyafuata maagizo haya yote ninayowapa leo. 6 eKwa kuwa Bwana Mwenyezi Mungu wenu atawabariki kama alivyoahidi, nanyi mtawakopesha mataifa mengi lakini hamtakopa kwa yeyote. Mtatawala mataifa mengi lakini hakuna taifa litakalowatawala ninyi.

Copyright information for SwhKC